#Njama #Yaliyojiri

Magongwa ya Mlipuko ni Njama ya Kupunguza Watu Duniani au ni Bahati Mbaya?

virus & red blood cells

Katika kila janga la kimataifa kunakuwepo na minongo’no na maswali yanayoleta utata juu ya kuamini uhalisia wa janga hilo na kuwa na mashaka nalo. Watu huwa wanahoji iwapo majanga haya ni sehemu ndogo ya mpango mkubwa wa kupunguza idadi ya watu duniani? Au ni bahati mbaya tu inayotokea kulingana na asili ya watu ili kupima uvumilivu wa binadamu?

Wakati watu wakiendelea kujiuliza kuna nini kinaendelea, tumegundua kwamba kuna hali ya kujirudia imetokea kwa miaka inayofanana. Hapa naongelea ile miaka ambayo tarehe 1 January ilianza siku ya Jumatano. Kuna mwaka 1992,1997, 2003, 2014, 2020 na 2025. Je hii ni bahati mbaya, Mungu ana jambo lake na wanadamu au ni mambo tu yanatokea?

Wacha tuangalia yaliyomo ndani ya miaka hii ili tuone kama ni mambo ya kupangwa au bahati mbaya inatokea.

1992: Mwanzo wa Kilele cha UKIMWI

Kufikia miaka ya 1990s, dunia yote ilikuwa tayari inahangaika na janga la UKIMWI ambalo lilionekana kupamba moto kuliko kawaida. UKIMWI tayari ulikuwepo tangu miaka ya nyuma, lakini 1992 ndiwo ulikuwa mwaka wa kipekee kwa ugonjwa huu.

Kampeni za UKIMWI duniani kote zilishika vichwa vya habari, na mamilioni ya watu walipoteza maisha kwa ugonjwa huu. Kuna watu waliamini kwamba ugonjwa huu umetengenezwa na serikali pamoja na matajiri ili kupunguza idadi ya watu duniani. Kwa miaka mingi sasa wanasayansi wamejitahidi kufanya majaribio kuthibitisha kwamba nadharia hizo si za kweli, pia wamekuwa wakijaribu kutengeneza dawa ya ugonjwa huu.

1997: Mlipuko wa mafua ya ndege (AVIAN Influenza H5N1)

Mwaka 1997 dunia ikatambulishwa kwa ugonjwa ulioitwa Mafua ya ndege au kwa lugha ya malkia AVIAN influenza. Ugonjwa huu kwa mara ya kwanza uligundulika huko Hong Kong na kusababisha hofu kubwa kwa watu maana ulionyesha kuweza kutoka kwenye ndege na kuhamia kwa binadamu. Asilimia kubwa ya watu waliopata ugonjwa huu walipoteza uhai kabla tiba haijaanza kufanya kazi.

Serikali zilihukumiwa na wananchi kwamba hii ni njama ili waweke vizuizi juu ya vyakula na usambazaji wa vyakula. Ingawa hakukuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi, ila hii ilionyesha kwamba dunia imeungana zaidi tofauti na ilivyokuwa zama za nyuma.

2003: SARS Janga lililobadili mtazamo wa dunia

Magonjwa ya Kupumua Makali Sana (SARS) yalijitokeza mwaka 2003, yakienea kwa haraka kutoka China hadi sehemu nyingine za dunia. Kulikuwa na zaidi ya kesi 8,000 zilizoripotiwa na karibu vifo 800. SARS ilitoa onyo la jinsi virusi vinaweza kuvuka mipaka haraka sana katika enzi ya utandawazi.

Nadharia nyingi ziliibuka kuhusu asili ya kirusi hicho, baadhi wakidai kuwa ni silaha ya kibaiolojia iliyokwenda mrama. Bila kujali asili yake, SARS ilisababisha serikali kufikiria upya jinsi zinavyokabiliana na magonjwa ya kuambukiza na kusababisha kuanzishwa kwa mifumo madhubuti zaidi ya kukabiliana na milipuko ya magonjwa.

2014: Mlipuko wa EBOLA

Mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi mwaka 2014 ulikuwa mkubwa zaidi katika historia, na kuua zaidi ya watu 11,000. Ebola, ikiwa na dalili za kutisha na kiwango kikubwa cha vifo, ilisababisha hofu katika mabara mbalimbali. Tena, wanaoamini nadharia za njama walidai kuwa Ebola ilikuwa sehemu ya njama ya kupunguza idadi ya watu Afrika au jaribio la silaha za kibayolojia.

Kinyume chake, jamii ya kisayansi ilijitokeza na kuunda matibabu na chanjo. Mlipo huo ulionyesha umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa, huku mashirika kama Shirika la Afya Duniani (WHO) na Madaktari Wasio na Mipaka yakichukua nafasi muhimu katika juhudi za kudhibiti mlipuko huo.

2020: Janga la COVID-19 kwa jina maarufu Tanzania ni CORONA

Hakuna mjadala wowote kuhusu milipuko ya kimataifa utakaokamilika bila kutaja janga la COVID-19. Likianza mwishoni mwa mwaka 2019 na kuwa janga kamili kufikia mapema mwaka 2020, kirusi kipya cha corona kilibadilisha dunia. Kufungwa kwa miji na machafuko ya kiuchumi yakawa hali mpya ya kawaida.

Kulikuwa na nadharia nyingi juu ya COVID-19 kuwa ni kazi ya binadamu ili kupunguza watu duniani. Na kuna nadhari za mataifa kama Tanzania zilisema janga hili halikuwa na uhalisia wowote. Hivyo hakukuwa na haja ya kujifungia ndani wala kutumia madawa ya gharama. Ilikuwa mwendo wa kujifukiza tu.

2025: Mwaka Umeanza Polepole na Ugonjwa wa HMPV

Kuongezeka kwa magonjwa ya mfumo wa kupumua ikiwemo virusi vya Human Metapneumovirus (HMPV) kaskazini mwa China kumezua wasiwasi mkubwa.

Haya yanajiri miaka mitano baada ya kuibuka kwa virusi vya Covid-19 nchini China, ambavyo vilisababisha janga la kimataifa na vifo milioni saba.

Mafisa wakuu wa afya wa China wamesema kuwa idadi ya maambukizi, hasa kwa watoto chini ya umri wa miaka 14, inaongezeka, lakini wamekana madai kwamba hospitali nchini humo zimejaa kutokana na virusi hivyo.

Maambikizi ya virusi hivi pia vimeripotiwa nchini India.

Tukiangalia hii pattern ya kutokea kwa magonjwa haya ni ngumu kutoona hali ya kujirudia. Sasa je ni kitu kinachotokea bahati mbaya au kweli kuna njama za kimya zinaendelea zinafanikisha magonjwa haya yatokee. Inawezekana pia ni kwamba magonjwa yanatokea tu katika vipindi hivyo bila kujali ni vipindi gani.

Swali hili linabaki kuwa la mjadala. Wakati wengi wanavyojadili kwamba milipuko hii ni matokeo tu ya asili ya ulimwengu wa kisasa wa kimataifa, wengine wanaendelea kutafuta majibu, wakijiuliza kama kuna zaidi nyuma ya matukio haya kuliko tunavyoambiwa.

Mwishowe, iwe ni njama ya kupunguza idadi ya watu au ni bahati mbaya ya wakati, jambo moja ni hakika: Dunia bado ipo katika hatari ya mizozo ya kiafya ya kimataifa. Kama historia inavyoonyesha, inachukua tu mlipuko mmoja kutuma mtikisiko kote duniani.

Magongwa ya Mlipuko ni Njama ya Kupunguza Watu Duniani au ni Bahati Mbaya?

Ni Kweli Marekani Walifika Mwezini?

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *