#Simu #Teknolojia

VPN Kill Switch ni Nini? na Unaitumia Vipi?

VPN kill switch

Nini kitatokea ikiwa vyumba yako haitakuwa na paa, vioo kwenye madirisha na hakuna milango? Itakuwa kama kutembea uchi sio? Basi unaweka siri yaliyo ndani ya nyumba yako na kuongeza ulinzi kwa kuweka paa, madirisha na milango.

Hivyo ndivyo internet unayotumia ilivyo bila matumizi ya VPN (Virtual Private Network). VPN ni mtandao binafsi ambao unaweka siri yale yote unayoyafanya online. Na ikitokea VPN unayotumia inapoteza uwezo wa kufanya kazi, basi VPN Kill Switch inaweza kutatua shida zako.

Katika ulimwengu wa sasa VPN zinatumika sana na kila aina ya watu walioko online. VPN zinasaidia kuweka siri yale yote wanayofanya watu online na pia inasaidia kupata access ya baadhi ya vitu vilivyozuiliwa kwa maeneo fulani.

VPN mara nyingi inakuwa kwenye simu au computer, lakini pia unaweza kuiweka kwenye router yako, ili kila kifaa kwenye mtandao wako kiwe na ulinzi wa VPN. Sasa iikiwa wewe ni mtumiaji wa VPN basi ni vyema ujue moja ya feature muhimu ya VPN inayoitwa VPN Kill Switch.

Kwa kuanza nikukumbushe kwamba VPN haifanyi wewe usijulikane mtandaoni. Ukiingia (login) Twitter au google, hizo kampuni zote zitaweza kutunza taarifa zako na kujua nini umefanya kwenye huduma yao.

Inachokusaidia VPN kufanya ni kwamba simu au computer yako haiunganiki moja kwa moja na server za huduma hizo. Badala yake zinafungua connection ya siri kutoka kwako kwenda kwenye server za hiyo VPN na kisha kwenye hiyo website. Hii ina maana ya kwamba ni ngumu kupata eneo ulilopo na kujua kifaa gani unatumia.

Pia inafanya iwe ngumu kwa mtu yeyote wa kati kuingia na kujua ni nini ulikuwa unafanya online. Wao wataona tu kifaa chako kimeunganika na serve ya VPN fulani. Ila nini umefanya ulipounganika nayo hawatojua.

VPN Kill Switch ni Nini?

Kill switch ni muhimu ziwepo kwa sababu VPN sio kitu kiishicho milele kuna muda huwa zinafeli kufanya kazi zake. Wakati mwingine inaweza kuwa upande wa kifaa chako ndiko kuna shida na kusababisha mawasiliano baina yako na VPN kukatika.

Ikitokea hali kama hiyo ya mawasiliano kukatika, ule usalama na ulinzi uliokuwepo sababu ya VPN unapotea. Kwahiyo kila kitu unafanya online kinabaki kuwa uchi. na hii si kitu uliyokuwa unataka. si ndiyo?

Kill Switch kama ilivyo kwenye mashine za kawaida kazi yake ni kuzima kila kitu. Kwenye vifaa vya mawasiliano kill switch inazima mpaka internet yenyewe ili kusiendelee kuwa na mawasiliano baina yako na mtandao.

Kwahiyo wakati kwa muda mfupi utakosa internet, ila utakuwa salama kwa kuwa data ulizokuwa unatuma kwa muda huo hazitaendelea kwenda hivyo hakuna mtu wa kati atakayeona vitu ulivyokuwa unatuma. Mara nyingi tunatumia VPN kuzuia mtu wa nje asione tunachofanya au ili tuweze kuufikia mtandao fulani, ili kukamilisha kazi zetu. Kwa sababu ya usiri huo ni muhimu kuwa na kill switch.

Bila kill switch kuwepo, huduma ulizokuwa unatembelea mtandaoni na mtu wa kati kama mtoa huduma wako ataweza kuona kila kitu unachokuwa unafanya pale ambapo VPN itakata mawasiliano.

Unaiwasha Vipi Kill Switch

Kulingana na VPN unayotumia na features zilizopo ndani ya VPN hiyo. Kuna baadhi ya VPN huwa hazina hii feature ya kill switch hivyo kill switch inabidi uwe wewe mwenyewe kuzima internet manually.

Nenda katika settings za VPN yako angalia kama kuna sehemu imeandikwa kill switch. Ikiwa hapo haionekani basi huenda imefichwa ndani zaidi kwenye advanced settings. Kwahiyo nenda huko na uitaikuta hiyo kill switch.

VPN Kill Switch ni Nini? na Unaitumia Vipi?

AI Kuwa Mshauri wa Fedha kwa Vijana

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *