#Teknolojia

Ross Ulbricht: Mtaalamu wa Silk Road Aliyeushinda Mfumo

ross ulbricht silk roads

Vijana wengi wakiwa umri wa miaka kati ya 20 mpaka 30 huwa ni kipindi wanajitafuta kiuchumi mpaka kiakili. Ni kipindi cha kufanya makosa na kurekebisha maana nguvu na muda bado upo. Vijana wengi hasa mtandaoni huona mengi na kuwa na ndoto za kubadili dunia na kuwa matajiri. Hii ndiyo ilikuwa ndoto ya kijana wa Texas, huko marekani bwana Ross Ulbricht.

Ilikuwa tarehe 29 May 2015 katika federal court pale New York ambapo ilitangazwa hukumu isiyo ya kawaida ikihusu usafirishaji wa madawa ya kulevya. Kijana Ross Ulbricht alihukumiwa vifungo viwili vya maisha bila msamaha. Mama yake mzazi katika moja ya Interview alisema, “Wanamhukumu mwanangu kwa kosa alilofanya akiwa na miaka 26.”

Kila rafiki na ndugu aliyemfahamu Ross alisema jamaa ni mtu wa kila mtu. Ni rafiki wa kila mtu na ni mtu mwema sana, lakini ni kitu ambacho kigumu kuelewa baada ya yeye kujulikana kwamba ni mhalifu. Sababu ya Ross Ulbricht kupewa hukumu kali kiasi kile, ni aliunda website.

Website ambayo ni mfumo wa kuuza bidhaa ya aina yoyote bila makato ya kodi na bila mtu kujua mnunuzi ni nani na muuzaji ni nani. Kila kitu ndani ya hii website kilikuwa siri mpaka majina hayakutumika ya kweli na mfumo wa malipo ulikuwa ni crypto currency inayoitwa BITCOIN.

Kiufupi Ross alitengeneza mfumo ambao ulikuwa ndoto ya mtu yeyote aliyefanya biashara haramu kama uuzaji wa silaha bila leseni au uuzaji wa madawa ya kulevya. Ndani ya mfumo huu kulikuwa na madawa zaidi ya aina 13,000.

Kuanzia 2011 mpaka 2013 Ross alikuwa adui wa jamii namba moja, na ilisemekana ndani ya miaka miwili website yake Silk Roads ilitengeneza zaidi ya $180 milioni. Ross alikuwa ni mkereketwa wa chama cha Democrats ambacho kimetoa maraisi kama Barack Obama na Joe Biden. Aliamini katika watu kuwa huru na kuwa na maamuzi yao wenyewe ambayo serikali haihusiki.

Maisha yake yote tangu mtoto hayakuwa ya tabu, maana alikuwa na wazazi wote wawili ambao ni wajasiriamali. Baba alikuwa engineer wa kuchora ramani za majengo, hivyo pesa haikuwa shida kwao. Ross alipenda michezo kama American fooball, surfing na basketball. Pia alikuwa skauti aliyefikia cheo cha juu kabisa cha kuwa Eagle scout, hivyo kuwa kwamba mtu kama huyu atakuwa mharifu ni ngumu.

Akiwa na miaka 22 kijana mwenye akili nyingi alipata scholarship ya kwenda kusoma katika chuo cha PennState. Akiwa ndani ya chuo hiki ndipo maisha yake yanaanza kubadilika. Alikuwa mwanafunzi bora wa fizikia tangu elimu ya sekondari na akiwa chuo akabobea katika Masters in Material and Engineering. Alisoma sana kuhusu crystals na alikusudia kupata PhD katika sekta hiyo.

Ilikuwa katika chuo hiki ndipo alikutana na mpenzi wake Julia. Kwa miaka miwili Ross aliandika thesis yake juu ya Material science, lakini kila akipata muda alisoma na kuvutiwa sana na siasa za Marekani. Umri wake na yuko chuoni ni kitu ambacho vijana wengi kinawakuta. Ukiwa chuoni na ukikutana na wazo jipya kwako unajikuta unalipenda sana na kutamani kulifanyia kazi.

Kwa Ross hii haikuwa kitu cha kupita tu. Ilikuwa ni kitu alikitaka sana. Alijua nini anataka alipokutana na kazi za Ludwig Von Mises. Mwanauchumi na mwana nadharia kutoka Austria ambaye alitamburisha mwenendo wa LIBERITARIANISM kule USA.

Watu wanaomini katika mfumo huu wa maisha wanaamini kwamba serikali inawanyima watu uhuru wa kweli na serikali ndiye adui namba moja wa watu. Ross aliamini kwamba serikali haikutakiwa kuhusika na maisha ya watu kwa namna yoyote ile. Mwaka 2009 ndipo Ross alianza kuweka wazi mawazo yake na maono yake juu ya maisha ya watu na serikali.

Mwaka 2009 Ross aliamua kuachana kabisa na masomo, aliona hayamvutii na kuamua kujihusisha zaidi na kusoma siasa. Katika kipindi hiki alikuwa karibu sana na rafiki yake Donny ambaye pia alisoma pale PennState. Baada ya muda kidogo Ross alirudi kwao Austin Texas ambako alijihusisha sana na makundi ambayo hayakuitaka serikali ikae madarakani.

Mwaka 2010 Ross alitoka nyumbani kwa wazazi na kwenda kuishi peke yake kabla mpenzi wake Julia hajaja kujiunga nae. Kipindi wanaishi pamoja Ross alibadili kazi mara kwa mara, kuna wakati kwa muda mfupi alitulia. Huu ni wakati alipoanzisha kampuni yake ya Video Games. Alitengeneza game moja ambayo ilipata wawekezaji. Bahati mbaya game haikufanikiwa na kampuni ilikufa.

Wakati anatengeneza game pia alikuwa akitrade katika Forex na Hisa kisha baadae akawa muuza bima kwa miezi kadhaa. Zote hizo hakuona zinamvutia vya kutosha akabadaili tena na kuwa editor. Alionekana kuwa mtu ambaye hakujua nini anataka na mara kwa mara alifeli katika yale anafanya.

Ross alikuwa mtu aliyeamini ana mafanikio makubwa yanamsubiri mbele yake, na huku kufeli mara kwa mara kunamchelewesha. Ni katika kipindi hiki ambako alianza kuandika shajara. Aliandika kila kitu alichofanya na alichohisi. Rafiki yake Donny akaona amuokoe jamaa yake kwa kumuita wafanya kazi pamoja katika kampuni aliyoanzisha.

Kampuni iliitwa GOOD WAGON. Wao walikusanya vitabu vilivyotumika na kuviuza tena mtandaoni. Kampuni yao ilihitaji kuwa na website na kati yao hakuna aliyejua wala kuweza kuunda website. Ila Ross akasema atatengeneza website yao. Alijifunza na kutengeneza hiyo website bila shida yoyote na aliweza vizuri tu. Ross alikuwa mtu mwenye uthubutu na hakuogopa chochote.

January 2011, Donny alitakiwa kwenye safari ya kibiashara huko dallas na kumuachia biashara yote Ross. Kazi ya Ross ilikuwa kuhakiki vitabu 50,000 ndani ya stoo yao. Ilikuwa kazi kubwa, lakini kila akipata nafasi Ross alikaa kwenye computer yake na kufanya kazi zake mpaka akawa anajisahau. Ilibidi ampigie simu Donny na kumuomba msamaha kwa kushindwa kufanya kazi, lakini pia amepata wazo ambalo linahitaji muda wote.

Wazo la Kubadili Maisha ya Ross Ulbricht

Hili ndilo wazo Ross alikuwa akisubiri kwa muda mrefu sana. Hapa ndipo aliona mafanikio yako kabisa mlangoni kwake yanasubiri ayafungulie tu yaingie ndani.

Siku hii aliandika kwenye shajara yake kwamba wazo lake ni kuunda website. Website ambayo itaruhusu watu kuuza na kununua vitu bila utambulisho wao wa kweli. Akaandika amesoma hii teknolojia kwa muda ila anahitaji mfumo wa biashara. Hii itakuwa jukwaa la kuuza mtandaoni ambalo haliguswi na sheria za nchi na kodi za aina yoyote.

Mwanzo aliita hii website Underground Brokers, lakini baadae akaona jina Silk road linafaa zaidi. Jina hili lilitokana na njia za wafanyabiashara waliofanya biashara kati ya Europe na Asia miaka 2000 iliyopita. Julia ndiye mtu pekee Ross aliweza kumwambia ukweli juu ya kile anakifanya.

Silk road ilikuwa wazo zuri ila bado Ross alikuwa na changamoto moja. Anawezaje kuficha utambulisho wa watu online?

Ukienda sehemu kama Alibaba kununua bidhaa kuna namna mbili wanaweza kutambua kwamba ni wewe.

  1. IP Address. hii ni anwani ya computer yako ambayo inaonyesha mpaka eneo ulipo unapotumia internet.
  2. Credit Card. Credit card utakayotumia kufanya malipo lazima itakuwa na jina lako hivyo ni rahisi kujua kwamba ni wewe umenunua bidhaa.

Hivi vitu viwili ilibidi Ross afanye kila namna apate mbadala. Hapa ndipo akakumbuka matumizi ya VPN na Tor Browser. Hivyo Ross akaweka kwamba huwezi kuingia kwenye website yake bila kuwa na Tor browser. Hii ni browser ambaye inabadili IP Address yako na location uliyopo.

Na kuhusu malipo aliweka kwamba utalipia kwa Bitcoin. Bitcoin ni mfumo wa malipo ambao hautumii utambulisho wako binafsi na hakuna serikali wala mtu mmoja anayeweza control taarifa za huko kwa namna yoyote. Mtu yeyote anaweza kuitumia bila kizuizi cha kuweka utambulisho wako.

Tarehe 15 January 2011, website ya Silk roads ikawa wazi kwa jamii mtu yeyote aweze kuitumia. Kabla ya kuiweka live alimuonyesha Julia kila kitu website ikiwa haina bidhaa yoyote. Juliana aliona ni kama wazo zuri sababu hakujua nini kitauzwa huko.

Kwa kujaribu Ross alianza kwanza kwa kuuza uyoga aliozalisha yeye mwenyewe na watu wakapenda sana namna ya malipo na ile kuto kujulikana. Alifanya hivi ili kuvutia watu watumie website yake. Uyoga aliuza huku si huu wa kawaida. Ni uyoga wenye asili ya madawa ya kulevya.

Hii ilikuwa sheria ya kwanza aliyovunja bwana Ross Ulbricht. Ndani ya siku chache alifanikiwa kuuza kilo 5 za huu uyoga.

Kipindi website imekuwa live, kulikuwa na mtafiti Nicholas Christen, aliyebobeba katika usalama wa computer alikutana na hii website Silk Road. Nicholas alianza kufanyia utafiti hii website kwa ajili ya Carnergie Mellon University. Alifanya majaribio live kuonyesha kwamba unaweza kutumia Bitcoin kulipia bidhaa na ukapokea mzigo wako.

Utafiti huu mubashara ulifanya watu wengi waifahamu na kuanza kutumia Solk Road. Katika forum mbali mbali watu waliongelea Silk Road pekee kwa muda.

Hii ilifanya wauzaji wengi wa madawa waanze kutumia silk road kuuza madawa yao. Madawa kama bangi, heroine na coccaine vyote viliuzwa huko. Walitumia njia ya post kusafirisha bidhaa zao. Hakukuwa na njia salama na uhakika zaidi ambayo haikuwa na maswali mengi kuzidi posta. Mtu anayenunua na kuletewa mzigo kwa posta kule marekani analindwa na sheria. Hivyo ikiwa mzigo umeletwa na akagundua polisi wapo anaweza kataa kusaini kupokea mzigo na hakuna sheria itamhukumu.

Katika mauzo yote ndani ya Silk Road, Ross alichukua asimili 7% kama kamisheni ya kila mauzo. Mafanikio ya Silk Road yaliongezeka baada ya blog ya Gawker ilipoandika kuhusu silk roads tarehe 1 June 2011.

Kuanzia hapo mauzo ya Silk Road yaliongezeka kwa kiasi kikubwa. Kulikuwa na akaunti mpya takribani milioni moja zilizojiunga kutumia Silk Road ndani ya siku chache. Mafanikio haya yalikuwa ghafla mpaka Senator Charles Schumer wa chama cha democrats alitoa ombi kwamba vyombo vya dola viifungie website hii.

Ilikuwa kama tamko dogo, lakini ndilo tamko lilifanya Silk Road ianze kuangaliwa sana na taasisi zote za kodi na usalama za Marekani. Kuanzia CIA, FBI, NSA, DEA mpaka IRS walianza kuichunguza kwa ukaribu mno Silk Road. Hapa ndipo Ross Ulbricht alianza kuwa adui namba moja wa Marekani.

Wakati vyombo vya dola vinamtafuta Ross, Ross anapigwa na shambulio lingine kwenye website yake. Ross aliunda hii website yeye mwenyewe bila uzoefu wa kutosha, hivyo kulikuwa na changamoto kadhaa za kiusalama kwenye website yake. Wadukuzi walianza kuona hizi changamoto na kuzitumia kwa manufaa yao.

Wadukuzi waliodukua website yake mara kwa mara walimwambia alipe ili waachie website hii. Kwa sababu hakujua kuzuia na hakutaka watu wajue mara nyingi aliishia kuwalipa.

Mwishoni mwa mwaka 2011, Ross aliachana na Julia baada ya kuona anazingatia sana Silk Road kuliko mahusiano yao. Hii ilikuwa kama Ross katolewa pingu mikononi mwake. Aliamua kuondoka na kuhamia San Fransisco mwanzoni mwa mwaka 2012. Alienda huku kama ndoto ya tech bros wengi, kwamba San Fransisco ndiko sehemu sahihi ya kupata utajiri. Ross alijiona akitengeneza $100 milioni kwa mwaka.

Akiwa San fransisco aliishia na jamaa wengine, lakini yeye alichagua chumba kidogo na kujifungia huko muda mwingi akifanyia kazi website yake. Wauzaji na wanunuzi walijua wanawasiliana na mtu anaitwa ADMIN, lakini Ross alitaka kujulikana na kuacha legacy hivyo alitaka kubadili jina.

Akaamua kujiita DREAD PIRATE ROBERTS au DPR. Aliiga hili jina kutoka kwenye movie ya The Princess Bride ya mwaka 1987. Alikuwa akizima tu computer yako anakosa rafiki na mtu wa kuzungumza naye. Hakujua anaweza kumuamini nani na hakujua nani anaweza kumuajiri amsaidie.

Mwanzoi mwa mwaka 2013 mauzo yalifika $300,000 kwa siku. Wadukuzi waliongezeka na wauzaji wakorofi hawakuwa wanalipa kamisheni zao. Kukosa marafiki na mtu wa kuongea kulifanya ajione kama boss wa mafia. Maana muda wote aliishia kwa wasiwasi na bila mtu wa kumuamini.

Ni mpaka siku moja alipokutana na mtu online aliyejiita NOB. Huyu aliweza kujifanya rafiki mzuri na Ross akamuamini. NOB alijifanya kama mtu muhimu sana wa Cartels huko mexico na aliweza kufanya Chochote.

Ross aligundua mmoja wa wauzaji anaiba Bitcoins kwenye mfumo wake, hivyo akaomba msaada kwa NOB. NOB akauliza kama anataka huyu mtu auwawe, apigwe au aende tu kumsalimia. Ross alisema apigwe na kurudisha bitcoins alizoiba.

Siku chache baadae Ross akabadili mawazo na kumwambia amtoe kabisa uhai.

Hili lilikuwa kosa la kwanza la Ross. Maana alitoa maagizo haya kwa mtu asiyemjua. Kitu hakujua ni kwamba huyu alikuwa agent wa DEA aliyejifanya rafiki wa kweli anayetaka kumsaidia. NOB ni mmoja wa agents ambao walikuwepo ndani ya Silk Road wakitaka kumkamata Ross.

Hili kosa si kitu kilicho mkamatisha bwana Ross. Maana mpaka hapo hakuna taarifa binafsi iliyoweza kuwajulisah kwamba Dread Pirate Roberts ni Ross. Kwahiyo bado alikuwa salama.

Aliyekuja kupata kitu cha kumakamatisha Ross ni agent mmoja katika taasisi isiyotegemewa. Alikuwa agent wa IRS ambayo ni sawa na TRA hapa Tanzania. Huyu hakuwa na ujuzi wa udukuzi wala vitu kama hivyo.

Wakati Ross anaunda Silk Road alifuta kila aina ya matangazo alifanya mtandaoni kuhusu silk roads. Sehemu zote alipoongelea silk roads alifuta kila kitu. Ila tunajua unaweza kufuta matatizo yako 99 katika 100 na hili moja ndilo ikawa kifo chako.

Huyu agent aliipata email ya Ross Ulbricht katika moja ya searches zake ndani ya google. Ingawa vyombo husika havikusema ni namna gani hii google search ilihusika na silk road, ila hii ndiyo ilimkamatisha Ross. Baada ya kupata hii email sasa uchunguzi ukaanza kufanyika kwenye mitandao ya kijamii ya Ross Ulbricht.

Maoni yake mtandaoni yalihusiana sana na tabia za DPR. Hivyo Ross akawa mtuhumiwa wa kwanza aliyeanza kufuatiliwa kwa ukaribu.

September 2013 huko San Fransisco kuna agents walipewa kibali cha kuanza kumfatilia Ross kwa ukaribu. Alikuwa agent wa kike na kiume ambao walimfuata Ross katika maktaba moja ambako Ross alipenda kufanyia kazi.

Alipenda kwenda maktaba sababu ya ukimya na kuficha IP address yake hata mtu akimfuatilia asijue wapi anaishi. Akiwa hapo aliingia kwenye mfumo wake kama kawaida na kuanza kuchat na watu wake. Ghafala alishangaa pembeni kuna mwanamke na mwanaume wanagombana.

Alipogeuka tu kuangalia yule mwanamke alivuta laptop ya Ross na yule mwanaume akamuweka Ross chini ya ulinzi.

Hii laptop ilikuwa muhimu isizime wala kutoka (log out) kwenye mfumo. Sababu kikitokea chochote kati ya hivyo basi hiyo laptop haitakuwa na msaada wowote kwao. Hapa ndipo walikusanya ushahidi wa kutosja ambao ulitumika mahakamani kumtuhumu Ross.

Pamoja na jitihada zote za kumuondolea hukumu Ross, mwanasheria wake alishindwa hii kesi. Wazazi na dada yake Ross walibaki kushangaa ndugu yao ndo huyu wanayemfahamu au kuna mwingine?

Siku ya hukumu ilikuwa tarehe 4 January 2015 ambapo Ross Ulbricht alihukumiwa vifungo viwili vya maisha bila msamaha akiwa na miaka 32. Ametumikia kifungo hicho mpaka January 2025 ambapo Raisi Donald J Trump kampa msamaha wa Raisi.

Ross Ulbricht: Mtaalamu wa Silk Road Aliyeushinda Mfumo

SEHEMU 1: Nyota ya Mrembo Aliyezikwa Hai

3 Comments

  1. Amon Aron
    24th Jan 2025 Reply

    AmaZing

  2. Saimonbey
    25th Jan 2025 Reply

    Story ya kumkomboa kijana w kiafrika kuamka kimawazo big up sana kaka ,

    • habaritech
      26th Jan 2025 Reply

      Pamoja sana mtaalamu. Nitaendelea kuandika nyingi za namna hii.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *