Kuanzisha Biashaya ya Mtandaoni na Mtaji wa Tsh. 250,000

Mapinduzi ya kidijitali Tanzania na Afrika kwa ujumla yameleta mabadiliko ambayo hayakutegemewa kwa wajasiriamali wa bara la Afrika. Afrika ikiwa na watumiaji wa internet milioni 500 na malipo kwa njia ya simu yakizidi kupamba moto, huu unaweza kuwa wakati mzuri kwa watu kuanzisha biashara ya mtandaoni.
Hii ni kwa sababu imekuwa rahisi na nafuu sana kufanya biashara mtandaoni. Ikiwa unauza bidhaa ulizotengeneza mwenyewe, bidhaa za kidijitali au bidhaa zozote zinazouzwa sana kwa wakati huo, nadhani unaweza kuanzisha biashara yako kwa kiasi cha Tsh. 250,000 tu na kuikuza polepole.
Kwanini Ujasiriamali wa Kidijitali ni Dhahabu kwa Afrika?
Uwepo wa simu janja (Smartphone) za bei rahisi na majukwaa/mitandao kama Whatsapp, facebook na TikTok imefanya iwe rahisi kwa kila mtu mwenye internet kumiliki biashara. Tofauti na mfumo wa kitamaduni wa biashara za zamani zinazohitaji eneo la biashara mpaka malipo ya kodi ya pango, biashara ya mtandaoni inahitaji gharama ndogo mno ya kuanzisha biashara.
Hii ndiyo inafanya biashara za mtandaoni ziwe sahihi kwa Waafrika wa hali ya chini kuweza anzisha biashara zao wenyewe. Kitu ambacho wanaweza ukifanya wakiwa mahali popote wakiendelea na kazi zao. Kwa sababu biashara ya mtandoni unaweza kuifanya kama part time na baadae ikiwa na faida nzuri ikawa full-time.
Kuna vitu ambavyo hufanyika katika biashara za kawaida ambavyo unaweza kuvifanya online. Kuna hivi vitu vitatu;
- Dropshipping/Udalali/Winga
- Freelancing/Kibarua
- Bidhaa za Kidijitali
Kati ya chochote utakachochagua kufanya kuna hatua za kufuata ili kuweza fanikiwa nia yako. Ni hatua ambazo kwa kiasi kikubwa zinaendana katika kila kimoja ilichotaja hapo juu.
Hatua 1: Chagua Jukwaa Linalofaa na Lisiwe na Gharama Kubwa Kwako. Ikiwa Chini ya Tsh. 50,000 ni vizuri
Dropshipping / Winga
Hapa una machaguo mawili yanayoweza kufaa kulingana na wapi unataka kuuza, lakini kwanza nikuelekeza unaweza vipi kuwa Winga mtandaoni. Winga wa mtandaoni hana ofisi maalumu wala hakai na bidhaa au kuishika hiyo bidhaa.
Kazi yake ni kutafuta mteja na kujua mteja anataka bidhaa ipi, kisha anachukua taarifa zote za mteja na malipo yote anaenda kwa muuzaji. Kule kwa muuzaji anapeleka taarifa za yule mteja na malipo stahiki ya huyu muuzaji.
Hivyo muuzaji ndiye mwenye jukumu la kufunga mzigo na kuandika anuwani ya huyu mteja halisi na kusafirisha mzigo kumfikia mteja. Mfano simu inauzwa Tsh. 1,000,000 dukani. Wewe Winga ukauza kwa mteja Tsh. 1,100,000. Hii Tsh. 100,000 ni faida yako. Hapa unakuwa umekamilisha biashara.
Sasa katika kuwa winga mtandaoni unaweza kutumia majukwaa ya kuuza bidhaa au ukatumia mitandao ya kijamii kama instagram, tiktok na X.
Majukwaa ya Kuuza utatumia aidha shopify, Jumia au Jiji. Yote haya yanafaa katika kufanya hii biashara ya kuwa winga.
Unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama Tiktok na instagram ambako unaweza kupost bidhaa ambazo maduka mengine wanapost na kisha baadae ukapata wateja na malipo yakafanyika kwa namna ya malipo ya simu.
Ukitumia mitandao ya kijamii gharama yako itakuwa ni bando lako tu la internet. Ukitumia jukwaa la kuuza kama Jumia gharama itakuja pale unapouza ambako Jumia huwa wanachukua kuanzia asilimia 5% mpaka 15% inategemea na aina ya bidhaa.
Ukitumia shopify uwe umeuza au hujauza kila mwezi utalipia kiasi cha $29 ili kutumia jukwaa lao.
Freelancing/Kibarua
Freelancing naita kibarua kwa sababu huwa na kazi za muda mfupi mtu unafanya kwa wateja mbalimbali. Yani unakuwa unauza ujuzi wako kwa wako. Kazi za kibarua mtandaoni unaweza kuzifanya pia kutumia mitandao ya kijamii kwa kujitangaza kuhusu ujuzi wako na kujenga brand yako.
Au unaweza chagua kufanya ndani ya majukwaa ya vibarua kama Upwork au Fiverr.
Digital Products / Bidhaa za Kidijtali
Hii inahusiana na utengeneza au ukusanyaji na uuzaji wa bidhaa kama eBooks (vitabu), templates za website, photoshop au madarasa ya topic mbalimbali.
Hivi vyote ni vitu ambavyo unaweza kuviuza mtandaoni na watu wengi wana nunua. Mfano kwenye eBooks zinaweza kuwa za mafunzo mbali au zikawa stori. Kwenye eBooks mfano mimi nimeuza magazines mbalimbali, nimeuza vitabu vya mafunzo kama (Namna ya Uagizaji Bidhaa Kutoka China, Namna Sahihi ya Kuchagua Computer ya Kununua na Uchambuzi wa Kampuni na Ununuzi wa Hisa Katika Soko la DSE)
Si hivyo tu unaweza kuuza vitabu vya Stori kama hii stori (Nyota ya Mrembo Aliyezikwa Hai) na hizi stori unaweza andika na kupost ndani ya website yetu ya Habaritech kipengele cha Stori na Sisi.
Hizo zote hapo ni link za kuweza kupata hizo eBooks.
Pia unaweza kuuza madara mbalimbali kupitia jukwaa kama UDEMY
Hatua 2: Fanya Matangazo Kama Mtu Mwenye Uzoefu (BURE)
Hakua mtandao au mtu atakufanyia matangazo bure. Lakini kuna namna unaweza kutumia mitandao ya kijamii na watu wakaweza kukufanyia matangazo bure bila wao kujua.
Kwanza cheza vizuri na algorithm za mitandao ya kijamii. Tumia mitandao kama Tiktok ambayo inaonyesha kuwa rahisi video na picha kwenda viral. Kadiri watu wengi wanapoona content zako kuhusu hizo bidhaa ndivyo unavyoongeza nafasi ya kupata wateja.
Katika mitandao ya kijamii penda kuwatumia watu wenye followers 100 hadi 1000. Fanya sana engagement na watu wa namna hii, ukishare content zao nao pia watashare zako. Akaunti nyingi zinaposhare content yako inakupandisha wewe juu zaidi kuonekana na watu wengi.
Hivyo ndivyo unaweza kuwatumia watu bure kukufanyia matangazo.
Hatua 3: Chagua Namna ya Malipo
Kulingana na unauza bidhaa za aina gani na hasa kwa watu gani jitahidi uwe namna nyingi za malipo ili usikose wateja. Mfano unakutana na wateja vijana watataka kulipa kwa Cryptocurrency, basi hakikisha unayo namna ya kupokea aina hiyo ya malipo.
Wapo wazee ambao watataka kulipa kwa njia ya simu pia hakikisha una namna rahisi ya kupokea malipo ya simu na hata ya benki. Muhimu zingatia kwamba namna ya malipo uliyo nayo haimuumizi sana mteja na wewe mwenyewe ili faida iendelee kuwepo.
Hatua 4: Usiache Kupost, Kuwepo Online na Kuendelea Kuboresha
Mtandaoni kila siku kuna mambo mapya na watu wapya. Hivyo unatakiwa kuhakikisha walau kila siku unaweka post moja kwenye akaunti zako ili watu waendelea kujua kwamba upo na waweze kukuamini.
Hakuna mteja atakuamini wala kununua kwako ikiwa makosa madogo kama kutoweka bei ya bidhaa au kuchelewa kujibu ujumbe wake na hata kukosa namna ya kuwasiliana na wewe yanakuwepo.
Hivyo ni muhimu kujenga uaminifu na kuwa active muda mwingi kwenye mtandao au jukwaa unalochagua kutumia.
Kuna watu ambao wanafanya hivi vitu mtandaoni na wameweza kufanyikiwa kwa kiasi kikubwa. Nitaweka majina yao hapa chini na link za akaunti zao mtandaoni.
Kundi la Mawinga
- Goodluck Maleko (Anauza Laptops)
- Isaac Chengula (Anauza Computer na Vifaa vingine vya elekroniki)
Vibarua
Kundi la Bidhaa za Kidijitali
Vitu vya Kuepuka na Kuzingatia
Kuna muda hutopata matokeo unayotegemea, usikate tamaa inatakiwa ujifunze namna ya kuboresha na kutafuta namna mbadala wa kuweza kupata wateja.
Unapoangukia kwenye mtego wa kukosa wateja usianze kufanya matangazo kwa lazima mpaka ukatumia gharama kubwa mno kwenye kufanya matangazo.
Jitahidi kuboresha biashara yako ifanyike kwa whatsapp na simu maana wanunuzi wengi wa Afrika wanatumia simu kufanya manunuzi mtandaoni.
Kitu usiache kufanya ni kufanya tafiti ya masoko. Usiuze bidhaa unayotaka wewe kuuza. Uza kitu ambacho jamii inayokuzunguka inahitaji. Usiuze mashine ya kufulia nguo kwa jamii ambayo haina umeme. Jamii hiyo inahitaji vifaa vya kuwapatia kwanza umeme.
Kuanzisha biashara mtandaoni Afrika sio tu inawezekana bali inafaida kubwa. Muhimu usiwe mtu wa kukata tamaa, uwe na ubunifu wa hali ya juu, uwe mtafiti na uwe na Tsh. 250,000 itakusaidia kuanza. Afrika sasa hivi ni kama imepata mlipuko wa watu wanaotumia mtandao na ni wakati mzuri kwenda na huu mfumuko.
Je, uko tayari kuanzisha biashara yako mtandaoni? Weka jibu lako au wazo lako la biashara kwenye comments hapo chini tuanze pamoja.