#Artificial Intelligence #Teknolojia

Kwanini Utatuzi wa Artificial Intelligence Afrika Unahitaji Data za Afrika? Kuvunja Ndoa na Ubaguzi wa AI wa Magharibi

artificial intelligence

Mapinduzi ya Artificial Intelligence (AI) yanabadilika sekta zote za uchumu na binafsi duniani, lakini kwa Afrika bado kuna changamoto kubwa moja. Modeli nyingi za Artificial Intelligence zinazotumika sasa hivi zinatumia mafunzo ya datasets za nchi za magharibi.

Kitu ambacho kinaleta ubaguzi wa hali juu sana ikiwa mtu anataka kutumia kwa ajili ya biashara na watumiaji binafsi wa Afrika. Kwa spidi ya ukuaji wa teknolojia Afrika sasa hivi, ni muda wa Afrika kuwa na Artificial Intelligence ambayo inaendana kiuhalali kabisa na mazingira ya Afrika.

Gharama ya Kutumia AI za Magharibi

Wakati Emmanuel Adegboye (mhandisi wa software huko Lagos-Nigeria) anajaribu kuunda AI ya kutambua sauti na maneno kwa ajili ya Kiingereza cha Nigeria na wazungumzaji wa Pidgin, alikutana na changamoto inayohuzunisha.

AI zilizopo zimefunza kwa kiingereza kinachozungumzwa na Wamarekani na Ulaya. Hivyo ilikuwa ngumu kwa hizi AI kuweza elewa lafudhi ya kiingereza cha watu wa Afrika. “Mfumo mara nyingi ulikosea kuelewa misemo na maneno ya kila siku ya Wanaijeria. Wakati mwingi ilishindwa kutambua mazungumzo.”, alieleza Emmanuel katika moja ya mahojiano. Na hii si tatizo pekee au mtu pekee aliyekumbana na changamoto hii. Hii ni changamoto iliyopo Afrika kote.

Changamoto Zilizopo Sasa Hivi

Ubaguzi katika Artificial Intelligence sasa hivi upo katika nyenzo hizi

  • Ugumu katika utambuzi wa sura (facial Recognition). AI zilizopo sasa hivi huwa na wakati mgumu katika kutambua sura za watu wenye ngozi nyeusi hasa pale mtu anapozidi kuwa na ngozi ya rangi nyeusi kama watu wa Sudani.
  • Model za uchakataji wa Lugha (Natural Language Processing, NLP) zinapata shida kutambua lafudhi na lugha za Afrika.
  • Mifumo ya Kutambua (Computer Vision) inashindwa kutambua vitu maalumu kabisa vya Kiafrika.
  • Mifumo ya AI ya kifedha inashindwa kuchambua sekta zisizo halali za uchumi ndani ya Afrika na katika masoko ya Afrika.

Athari Katika Biashara na Uvumbuzi wa Afrika

Ubaya wa huu ubaguzi hauishii tu kwenye upande wa kiufundi wa hii mifumo. Biashara za Kiafrika zinazojaribu kutumia hii mifumo huwa katika hasara ya kiushindani. Utafiti wa 2023 uliofanyika na African AI Initiative uligundua kwamba asilimia 67% ya biashara za Afrika zilizojaribu kutumia AI kwenye biashara zao, ziliripoti kwamba kulikua na changamoto ya usahihi kwenye hii mifumo.

Tukiangalia kama fintech Starup ya Kenya FinPlus ambayo ilijaribu kutumia AI katika kufanya credit scoring. CTO wao Sarah Kimani alisema, “AI models zilizopo hazina msaada wowote kwa masoko yetu. Zinashindwa kutambua kipato kutoka sekta zisizo rasmi au mikopo ya kijamii tuliyonayo Afrika Mashariki. Vitu ambavyo ni muhimu kwa Afrika katika kufanya vipimo vya credit score.”

Kuunda Utatuzi kwa Data za Afrika

Njia inayohitajika iko wazi. Afrika inahitaji Artificial Intelligence ambayo imefundishwa kwa data za Afrika. Kuna mipango kadhaa ambayo tayari imeanza kuongoza njia.

Kuna taasisi kama Data Science Africa na African Data Hub zinaongoza juhudi za kuunda ukusanyaji wa data za Afrika kwa kuzingatia.

  • Ukusanyaji wa sampo mbalimbali za lugha kutoka Afrika.
  • Kutunza na kukusanya data za kitamaduni za Afrika.
  • Kukusanya taarifa za kiuchumi mahususi kabisa kulingana na eneo.
  • Kuunda database za sura za watu wa Afrika.

Kuna kampuni ambazo tayari zinaonyesha mafanikio kwa kutumia AI ambazo zimefundishwa na data za Afrika. Kuna project kama Amharic AI ya ethiopia ambayo imefikia usahihi wa 95% katika kutambua lafudhi na lugha kwa kuifundisha AI yao maalumu kabisa kupitia wazungumzaji wa lugha yao. Wakati huo huo AI za magharibi zilikuwa na usahihi wa 45% tu.

M-Pesa AI ya safaricom Kenya imeweza kuboresha utambuzi wa utapeli kwa 60% baada ya kuunganisha namna ya miamala ya Kenya katika AI zao.

Namna Developers wa Afrika Wanaweza Kuchangia

Ili kuweza fikia malengo ya kuwa na AI za Afrika, hizi project zinahitaji mchango mkubwa sana kutoka kwa developers wa Afrika na wanaweza fanya hivyo kwa;

  • Kuchangia Open-Source Projects, Inafaa developers wajiunge na mipangon iliyopo ya ukusanyaji data, kuchangia kutoa data zao walizokusanya katika hizi projects (muhimu ziwe data zisizotoa taarifa za watu.) na kuchangia katika kazi za kuweka label kwenye data zilizokusanywa.
  • Kuweka rekodi za muktadha wa Afrika, Hapa tunaongelea uhalisia wa maisha ya kila siku ya Afrika, kama changamoto za maisha yetu na utatuzi unaofaa. Pia kuchangia katika maadili ya AI katika taswira ya Afrika.
  • Kuunda Jamii. Kujiunga na makundi na jamii za waundaji wa AI Afrika ili kuweza changia maarifa waliyonayo, data mbalimbali na kuwafunza developers wachanga.

Safari Inayofuata

Kuunda AI zinazofuata data za Afrika sio tu kwa ajili ya usahihi wa data, hii inahusu uhuru wa kidijitali na uboreshaji wa uchumi wa Afrika. Hii inaonyesha kwamba Afrika itaweza kujitegemea. Kama ambavyo mkurugenzi wa Google AI Ghana Dr. Moustapha Cisse anasema, “Inabidi tuhakikishe kwamba uundaji wa AI Afrika unatatua matatizo ya Afrika na kuakisi taswira ya Afrika.”

Inachohitaji Afrika ni kuunda sera na sheria za ukusanyaji data ambazo zinaleta faida kwa Afrika. Lakini pia ili hii safari ifanikiwe inahitaji developers muda wote waweke jitihada za kuboresha hii mifumo wakishirikiana na serikali na wafanya baishara.

Tunavyuzidi kusogea ni vyema tutambue hizi si jitihada za kuwafikia magharibi katika AI, bali ni jitihada za kuunda kitu kipya ambacho ni kwa ajili ya Afrika na kinaeleweka na kutumika na Afrika kwa ajili ya manufaa ya watu wote wa Afrika.

Umekumbana na changamoto zipi katika matumizi ya AI hapa Tanzania? Unaweza changia hii mada katika comments hapo chini.

Kwanini Utatuzi wa Artificial Intelligence Afrika Unahitaji Data za Afrika? Kuvunja Ndoa na Ubaguzi wa AI wa Magharibi

Kuanzisha Biashaya ya Mtandaoni na Mtaji wa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *