#Teknolojia #Usalama

Kutoweka Data Zako Online, Hakuzuii Mitandao ya Kijamii Kuwa na Taarifa Zako

social media spying

Tunapenda sana kutumia mitandao ya kijamii. Ni kitu ambacho tangu kuanzishwa kwake jamii imekuwa ikihoji sana, juu ya namna wanatumia data zetu. Tumehoji wanazikusanya vipi na kuzitumia vipi. Ajabu ni kwamba mpaka leo hii bado hatusiti hata kidogo kutumia hii mitandaoya kijamii.

Tumekuwa watu wa kulalamika sana na kuhoji kila kukicha, lakini hatufanyi chochote kuacha kutumia hii mitandao. Wakati natumia TikTok ilikuja notification ikisema “People You May Know” yaani watu ambao inawezekana nawafahamu. Kuzingati asilimia kubwa ni watu ambao namba zao nimesave kwenye namba yangu.

Hivyo nikawaza inawezekana vipi, ikiwa nimeizuia TikTok kuona majina na namba kwenye simu yangu. Nikakumbuka kwamba hiyo ni Algorithm inafanya kazi. Kwa maana ya kwamba kuzuia TikTok kupata hizo namba kutoka kwangu ni kama kazi bure.

Nilichogundua ni kwamba ingawa hakuna uthibitisho moja kwa moja kwamba mitandao ya kijamii kama TikTok inaweza kuona taarifa kwenye simu zetu moja kwa moja kama hatujaruhusu, inawezekana wanakusanya data kwa wengine walioruhusu na kuzihusisha na sisi.

“People You May Know” Inakuja Vipi Bila Kuona Contacts wako?

“People you may know” ni feature ndani ya apps za mitandao ya kijamii kama TikTok, Facebook, Instagram na X. Kazi yake ni kujaribu kutengeneza marafiki wapya (uhusiano mpya) ili kukufanya wewe uendelee kubaki ndani ya app hiyo na kuifurahia. Hili ndilo lengo kubwa la hii feature. Kinachonipa wasiwasi juu ya feature hii ni namna inavyofanya kazi.

Ufanyaji wake kazi ni katika namna ambayo huenda inaondoa uzito wa wewe kuzuia app hiyo isipate ruhusa ya baadhi ya vitu kwenye simu yako. Mfano unaweza zuia hii app isione contacts zako, lakini bado itakuletea accounts ambazo namba zao unazo.

Kumbuka katika kukulete watu ambao unaweza kuwa unawafahamu wakati mwingine inaangalia namba za simu ulizonazo kama wamejisajili kwenye hiyo app. Ikiwa wamejisajili inawaleta kwako kama watu unaoweza kuwafahamu. Sasa tuangalie namna inafanya kazi kama hujaruhusu ione namba za simu kwenye simu yako.

Inatumia data za Wengine

Tuchukulia mfano kuna watu watatu (3). Charles, John na Vanessa wote wanatumia Tiktok. Charles peke yake kazuia Tiktok isione majina kwenye simu yake. Hawa wawili wengine wameruhusu. Wote wanafahamiana na kila mmoja ana namba za wengine wawili.

Tiktok inafahamu email na namba za simu za kila mmoja sababu walitumia wanapojiunga nayo. Charles alijiunga kwa siri na akaunti yake kaificha wenzake wasijue, lakini mara kwa mara akaunti ya John na Vanessa inaletwa kwake kwamba ni mtu anaweza kumfahamu.

Ilichokifanya TikTok ni kuangalia contact list ya John na Vanessa ambako ilikuta namba ya simu ya Charles. Kumbuka Tiktok tayari inaifahamu namba ya simu ya Charles sababu alitumia anapojiunga na huu mtandao.

Hivyo moja kwa moja inatengeneza uhusiano kwamba huenda Charles anafahamiana na John na Vaness na kuleta akaunti zao kwake kaman watu anaoweza kuwafahamu.

Watu Kuwa Kwenye Mtandao Mmoja

Ninaposema mtandao mmoja sio kama wote kutumia Vodacom au kuwa kwenye wifi moja, hapana. Maana yangu ni hii. Mfano Charles alikuwa na marafiki wengine Musa na Elia ambao wao ni marafiki wa John na Vanessa.

Charles hajafuatana mtandaoni kwenye akaunti za John na Vanessa, ila kwa sababu Musa na Elia mara nyingi wanakuwa tagged kwenye post za John na Vanessa basi moja kwa moja Tiktok inahusisha kwamba Charles atakuwa anafamiana nao. Kwahiyo inachofanya inamletea akaunti zao kwamba anaweza kuwa anawafahamu.

Tabia Yako Mtandaoni na Metadata

Apps za mitandao ya kijamii huwa zinaangalia namna utatumia huo mtandao. Vitu kama unatembelea akaunti ya nani, aina gani ya maudhui unaagalia sana na anayopost nani na hata eneo ulilopo kuna wakati inatumika.

Ikiwa akaunti unazo search mara kwa mara au kutembelea akaunti za watu waliopo kwenye contact list yako, basi utaletewa suggestion ya akaunti ambazo huenda moja kwa moja zinahusiana na wewe.

Wanakusanya Data kwa Siri Kupitia Akaunti Vivuli

Mitandao kama Facebook wamesha shitakiwa mara kadhaa kuhusu kuwa na akaunti vivuli za watu ambao bado hawajaruhusu mtandao huo kuona data zao na hata uwa hawaposti chochote. Wanachokifanya ni kukusanya data kutoka kwa watumiaji wengine. Data hizi ni zile zinazohusiana na wewe.

Baada ya kukusanya data hizo wanajenga akaunti kivuli kwa ajili yako. Akaunti hii ndiyo itatumika kuleta traffic kwako kulingana na vile vitu wanavyopost watu wengine.

Kwanini Hii Inaonekana Kuwa Usaliti kwa Watumiaji?

Hii mitandao inachukuwa data kutoka kwa wengine ambao wameweka taarifa zao mtandaoni, mfano contact list. Wakishachukua hizi data wanazihusianisha na wewe na kuleta vitu vinavyohusiana na wewe.

Kwahiyo hata taarifa kidogo wanazokusanya kwa wengine wanaweza kukujua wewe na kuunda akaunti kivuli ambayo itatumika kukufuatilia zaidi wewe.

Je, Kuzuia Permission Hakuna Maana? na Nini Ufanye?

Kuzuia permission bado kuna saidia sana sababu kuzuia permissions inasaidia kuwazuia hawa watu wa mitandao wasipate contact list yako moja kwa moja. Kitu ambacho ni kizuri sababu hautakuwa unauza namba zilizopo kwenye simu yako.

Kitu unaweza kufanya ni kupunguza kutumia namba yako binafsi ya simu na email yako wakati unajiunga na mitandao ya kijamii. Kama kuna kuwa na namna nyingine ya kujiunga na huo mtandao tumia hiyo.

Kama unaelewa na watu wenye namba yako na wote mnataka kitu kimoja waambie wao pia wazuie hizi apps kuona contact list zao. Hii inaweza kusaidia nyie wote kuendelea kuwa salama. Kama mtandao huo si muhimu sana kwako, jiepushe kutumia taarifa zako za kweli.

1 Comment

  1. John
    14th Apr 2025 Reply

    EFcJFbX ehgpd CfDk

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *