SEHEMU 1: Nyota ya Mrembo Aliyezikwa Hai

Jua lilikuwa linachoma kwa nguvu, likitawanya mwanga wake wa dhahabu juu ya jiji la Dar es Salaam. Katika kitovu cha mji, hoteli ya kifahari La Mirage Paradise ilionekana kama oasisi ya utulivu, ikikumbatia wateja wake kwa upepo wa bahari na harufu ya maua ya manemane. Hii ilikuwa hoteli maarufu kwa watu wa hadhi ya juu, sehemu ambayo maisha ya kifahari yalionekana kuwa kawaida.
Johnson alikuwa ameketi kwenye kona ya bustani ya hoteli hiyo, macho yake yakimtazama Janeth kwa mapenzi yasiyoweza kufichika. Jua lilipiga uso wa Janeth na kufanya ang’ale kama malaika. Janeth, mrembo wa asili mwenye ngozi nyororo kama hariri, alikuwa amevalia gauni nyekundu la kubana lililoonyesha umbo lake la kuvutia. Tabasamu lake lilikuwa kama miale ya alfajiri, likimvuta Johnson karibu naye kwa namna ambayo hakuweza kuielezea kwa maneno.
“Nashukuru kwa kunileta hapa, baby,” Janeth alisema kwa sauti laini, macho yake yakilegea na kumtazama Johnson kwa upole. “Mahali hapa ni pazuri sana.”
“Nataka uwe na furaha, mamii,” Johnson alijibu huku akimshika mkono wake kwa upendo. “Kila siku ninajisikia mwenye bahati kuwa na wewe.”
Wakiendelea kufurahia chakula cha jioni, hali ya utulivu ilivunjwa ghafla na sauti ya mtu aliyekuwa akiwakaribia. Ilikuwa ni Mark, rafiki wa muda mrefu wa Johnson, ambaye hakuwa amekutana naye kwa miaka mingi. Mark alifika akiwa amevalia suti ya kisasa, uso wake ukionyesha furaha ya kumuona rafiki yake wa zamani.
“Oi! Johnson! ,” Mark aliita kwa mshangao huku akimkumbatia kwa furaha. “Nimefurahi kinoma kuonana na wewe hapa. Nadhani hii ni bahati nzuri sana.”
“Kweli kabisa, bro,” Johnson alijibu kwa tabasamu la uchangamfu. “Karibu ujiunge nasi.”
Mark alikaa mezani pamoja nao huku akiwa na mpenzi wake, Rachel. Walifurahia mazungumzo mazuri, wakikumbuka nyakati za nyuma chuoni na kubadilishana habari za maisha yao ya sasa. Hata hivyo, kwa muda, Johnson alianza kuhisi hali isiyo ya kawaida. Aliona jinsi Mark alivyokuwa akimtazama Janeth mara kwa mara, macho yake yakiwa na tafsiri ya siri ambayo haikuwa rahisi kupuuza.
“Naona bro umevuta mrembo namba E kabisa,” Mark alisema huku akishushia na glasi ya wine. Wakati anasema hayo macho yake yalimkazia sana Janeth kwa jicho la tamaa. Maneno haya yalimchoma Johnson kama sindano ya baridi. Alijaribu kujizuia, lakini moyoni mwake, moto wa wivu ulikuwa ukianza kuwaka.
“Asante, Mark,” Janeth alijibu kwa tabasamu la kistarabu. Hata hivyo, ndani ya moyo wa Johnson, hali ya wasiwasi ilianza kuchukua nafasi ya furaha ya usiku huo.
Si kwamba Rachel hakuona kile kinachoendelea aliona ila akapuuza tu, maana alifahamu tabia za Mark ziko vipi. Si mara ya kwanza Mark kufanya kitendo cha ajabu cha namna ile. Kwa utani Johnson aligeuka na kumuuliza Rachel, “Vipi Shem mbona kimya hivyo? au bwana mkubwa huwa hataki uzungumze mkitoka out?”
Rachel aliishia tu kutabasamu bila kusema neno lolote. Kulikuwa na ukimya kwa sekunde kadhaa baada ya swali la Johnson, kisha Johnson akasema, “Unajua bro hawa wanawake sikuhizi ukiwaache wawe wanazungumza kila mara mkitoka unaweza kuaibika.” Kila mtu mezani akabaki kumshangaa Mark kwa maneno hayo. Ajabu ni kwamba hakuishia hapo akaendelea kusema, “Wanawake wako hapa kufanya yale tunataka sisi wanaume na kuhakikisha tunaridhike. Kama hapo wewe leo upo na Janeth usishangae kesho akawa na mimi,”.
Kwa maneno hayo Johnson hakuweza kuvumilia, alisimama kwa hasira na kumuamrisha Janeth waondoke mahali pale. Hakufurahishwa kabisa na yale aliyosema Mark.
Wakati wanatoka Mark aliendelea kuzungumza maneno mengine ya dharau kumsema Johnson kwamba ni dume suruali tu na nyuki wa mashineni hana lolote. Yote Johnson aliyapuuza mpaka pale Mark aliposema, “Demu mwenyewe unaringa naye malaya tu,”.
Hapo Johnson alishindwa kuvumilia, maana Mark aligusa moyo wake. Johnson akiwa mrefu na mwenye mwili mkubwa kuliko Mark alijua fika kwamba anamudu hiki kipande cha mtu chenye dharau. Alipomfikia Mark, Johnson alirusha ngumi moja tu iliyomfikia Mark na kumfanya aanguke na kuzirai hapo hapo kutoka kwenye kiti alichokalia.
Kwa hasira akamwambia Rachel, “Huyu si mwanaume sahihi kwako, tafuta mtu anayekufaa.” Kisha akaondoka zake na mpenzi wake.
Siku chache baadaye, Janeth aliandaa matembezi na marafiki zake wawili wa karibu, Linda na Joyce. Walikutana katika mgahawa maarufu katikati ya jiji uliojulikana kama Bella Vista Lounge. Janeth alikuwa ameazimia kuonyesha maisha bora aliyokuwa akiishi kwa msaada wa Johnson.
Linda, mwanamke mrefu na mwenye tabasamu la kuvutia, alikuwa wa kwanza kuzungumza. “Janeth, shoga yangu danga lako inaonekana linakulisha vizuri sana. Sasa hivi kila mtu anatamani kuwa kama wewe.”
“Ah, acha tu, Linda,” Janeth alijibu huku akicheka kwa dharau. “Si rahisi kama unavyofikiria. Inahitaji kazi na kujitoa.”
Hata hivyo, ndani ya moyo wake, Janeth alijua kuwa kazi aliyokuwa akiifanya ilikuwa zaidi ya kuonyesha tabasamu kwa umma. Maisha yake yamejaa siri na michezo ya hatari ambayo hakutaka mtu yeyote ajue.
Baada ya matembezi haya na rafiki zake, kila mmoja alishika njia yake kurudi kwake. Akiwa njiani Janeth alikutana na kijana aitwaye Brian.
Kijana wa umri mdogo na mvuto wa kipekee, na mara moja akamvutia Janeth. Mazungumzo yao ya kwanza yalikuwa mafupi lakini ya kina, yakifungua mlango wa uhusiano ambao ungeleta matatizo makubwa zaidi katika maisha ya Janeth.
“Umependeza sana, Janeth,” Brian alisema kwa sauti ya upole, macho yake yakimwangalia kama mtu aliyepata lulu ya baharini.
“Asante, Brian,” Janeth alijibu huku akitabasamu. “Natamani sana nipate muda zaidi na wewe, niweze kukufahamu vizuri.”Aliongeza kusema Janeth.
Brian kijana maji ya moto akaona hii ni kuokota dodo chini ya mnazi. Pisi kali kama hii imetoa ofa ambayo hawezi kuikataa.
Brian akasema kwa utani “Inawezekana, ila nyie watoto wazuri huwa mna mabwana zenu wenye hela nisije ondolewa duniani mimi.”
Janeth: (huku akicheka) Hapana bwana, mbona mimi niko single.
Brian: mmh! ya kweli hayo.
Janeth: Haki tena nakwambia, hapa mimi bado nakula hela za baba na za biashara zangu mwenyewe.
Waliendelea kuzungumza kwa muda kadhaa na kukubaliana lini tena wataonana.
Brian alikuwa bado anasoma chuo mwaka wa 3 pale chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Ni mtu aliyependa sana maisha ya raha na alijua kujiweka katika namna ambayo wadada wengi walivutiwa nae.
Tatizo la Brian ilikuwa moja tu, hakuwa na pesa ya kutosha kuishi maisha ya raha aliyoyataka na hakuweza kuwapeleka wanawake sehemu za starehe.
Kumpata Janeth ilianza kuwa nafuu kwa Brian. Maana binti alikuwa kapenda kweli na alikuwa tayari kufanya chochote kwa Brian. Alifikia hatua ya kuona kwamba anahitaji uhuru zaidi na Brian akaamua kumpangia nyumba nzima na akawa anamhudumia kwa mambo yote.
Wakati anafanya haya yote Janeth alikuwa akitumia pesa za Johnson maana Johnson alikuwa akimpa Janeth pesa nyingi sana bila kuhoji chochote.
Siku moja wakati Janeth akitoka kwa Brian wakiwa wameongozana kuna mtu mwingine alikuwa nyuma yao anatembe polepole sana.
Janeth na Brian hawakumzingatia na yeye pia hakuwa na muda nao. Janeth aliendelea kutembea na Brian kwa umbali kiasi huku wakiwa wameshikana mikono na kuendelea kupeana mabusu barabarani kama vile kwenye tamthilia za wafilipino.
Walifika mahali alipokuwa dereva wa Bolt anayemsubiri Janeth na ikabidi waagane na kuachana hapo. Jamaa aliyekuwa nyuma yao akawa anawaangalia huku akitamani yale maisha.
Macho yake yalionyesha matamanio ya hali ya juu sana wakati anamuangalia Brian akimkumbatia Janeth na kumbusu mdomoni kwa mahaba mengi wakati wanaagana.
Jamaa aliendelea kusogea karibu polepole ndipo akamtambua Janeth na kuhamaki akiita jina la mrembo Janeth.
Peter: Janeth! 😲
Janeth: Shem Peter!
Janeth alijibu kwa mshangao mkubwa na kumuacha hata Brian akishangaa imekuaje Janeth kamuita huyu jamaa Shem. Brian alibaki kujiuliza kwamba Janeth tayari alikuwa na bwana mwingine au vipi.
Peter nae akasimama akishangaa kuona kilichopo mbele yake. Peter ni rafiki wa muda mrefu wa Johnson. Wamesoma pamoja Chuo kikuu na sasa hivi walikuwa wanafanya kazi katika kampuni moja. Peter akiwa anafanyia kazi ofisi za Dar Es Salaam na Johnson akiwa director wa kampuni nchi nzima alikuwa akisafiri mara kwa mara.
Stori hii bado inaendelea katika sehemu mpaka ya 6. Ili kupata sehemu zilizobaki gusa namba hii ya Whatsapp +255753607400.
Anonymous
31st Jan 2025Waiting for part two
habaritech
02nd Feb 2025Muendelezo wa Part two mpaka 6 unapatikana kwenye group letu la Whatsapp wasiliana nasi kwa Whatsapp https://wa.me/255753607400